MASKUOTA UTANGE MOMBASA WAFURUSHWA SHAMBANI


Familia moja kule Utange Mombasa imesalia bila makao baada ya majumba yao yalioko kwenye shamba lenye utata kule Utange Mombasa kubomolewa Chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa Polisi.

Akizungumza na wanahabari baada ya kufurushwa kwenye shamba hilo lenye ekari 28, Darious Kazungu Mwaro amesema kwamba kwa sasa ahawana pa kwenda baada ya polisi kwa ushirikiano na bwenye anayedai kumiliki shamba hilo kuwavamia na kuteeketeza majumba yao.

Aidha Bi Esther Kalume amesema kwamba ni jambo la kutamausha kwamba licha ya wao kuwasilisha kesi hio mahakamani, agiza la mahakama limekiukwa, na wote kufurushwa shambani humo na sasa hawana pa kwenda.

Haya yanajiri huku utata wa mashmba ukisalia kuwa donda sugu katika ukanda wa Pwani