Mashirika ya kutetea haki za binadam yataka shule kufungwa ikiwa visa vya Corona vinaongezeka.


Shirika la kutetea haki za binadam Muhuri katika kaunti ya Lamu limetoa wito kwa waziri ya elimu nchini kuzifunga shule kwa mara ya pili ikiwa janga la corona limeingia wimbi la pili maarufu second wave ili kudhibiti msambao wa virusi hivyo.

Afisa wa shirika hilo Habib Ali amesema kuna hatari kubwa kwa wanafunzi wa darasa la nne, nane na kidato cha nne walio shuleni kwani baadhi ya shule Lamu hazifati maagizo ya kudhibiti msambao wa virusi.