Maseneta wakaidi Jubilee kuendelea kuandamwa


Masaibu yanazidi kuwaandama maseneta wa Jubilee waliokosa kuhudhuria mkutano aliouitisha rais Uhuru Kenyatta wiki moja iliyopita katika ikulu hapa Nairobi

Seneta wa Tharaka Nithi ambaye pia ni naibu spika Kithure Kindiki ndiye anayeandamwa leo, tayari hoja ya kumbandua ikiwa tayari kuwasilishwa kesho, duru zikiiarifu Radio Citizen kuwa huenda seneta wa Uasin Gishu Margaret Kamar ndiye anapigiwa upatu kuchukua nafasi hiyo

Kiranja wa wengi katika bunge la senet Irungu Kangata anasema Kindiki ni miongoni mwa maseneta waliokaidi wito wa rais ambaye ni kiongozi wa chama tawala

Wengine wanaolengwa ni seneta wa Nandi Samson Cherargei anayepaswa kufurushwa kutoka kamati ya sheria akiwa mwenyekiti, sawa na seneta wa Laikipia John Kinyua ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ugatuzi

Seneta mteule Millicent Omanga pia analengwa akiwa kwenye kamati ya uhasibu wa umma, sawa na mwenyekiti wa kamati ya fedha seneta wa Mandera Mohamed Mohamud

Barua zao yamkini ziko tayari kuwasilishwa kwa spika Kenneth Lusaka leo.