Maseneta wakaba koo KEMSA


Afisa mkuu wa shirika la kusambaza dawa nchini KEMSA Dr. Jonah Manjari amekosa kuwasilisha stakabadhi kuhusu matumizi ya fedha za bajeti ya mwaka wa kifedha 2017-2018 na 2019-2020 kama alivyoagizwa na kamati ya seneti kuhusu afya.

KEMSA hata hivyo amewasilisha stakabadhi kuhusu matumizi ya fedha zilizotumika katika ununuzi wa vifaa vya kukabiliana na janga la corona nchini japo pia kwa kuchelewa.

Kamati hiyo inayoongozwa na seneta Mary Seneta imetaja hatua hiyo kama ishara ya kutoheshimu bunge.

Maseneta Ledama Ole Kina, Fred Outa na Millicent Omanga wameitaka KEMSA kufahamu kuwa fedha inazotengewa ni za umma hivyo basi ni muhimu kufahamu jinsi fedha hizo zinavyotumika.