Maseneta kuamua mgao wa kaunti


Maseneta alasiri ya leo wanatarajiwa kuamua mbinu itakayotumiwa katika ugavi wa raslimali kwa serikali za kaunti.

Kwa mujibu wa mbinu mpya iliyopotishwa na kamati ya bunge la senate kuhusu fedha, kaunti ya Wajir itapoteza shilingi bilioni 2 Kwa bajeti yake, Marsabit shilingi bilioni 1.9, sawa na Mandera, Garisa shilingi bilioni 1.6, Tana River bilioni 1.5, Mombasa bilioni moja miongoni mwa kaunti zingine kadhaa.

Ni mbinu ambayo imepingwa vikali na maseneta ambao kaunti zao zinapoteza pesa huku wakisema hatua hiyo itahujumu maendeleo katika kaunti hizo.

Seneta wa Makueni, Mutula Kilonzo Jnr, Fatuma Dullo wa Isiolo na Ledama Ole Kina wa Narok wamepinga vikali hatua hiyo na kusema kamwe hawatokubali kaunti zao kupoteza pesa.

Hata hivyo katika mbinu hiyo ambayo inazingatia asilimia 18 Kwa wingi wa watu, masuala ya afya asilimia 20, kilimo asilimia 12, ukubwa wa eneo asilimia 4 pia imefaidi kaunti 29.

Kaunti ya Nandi ndiyo itafaidika pakubwa na mbinu hiyo huku ikipata shilingi bilioni 1.3, Uasin Gishu ikipata shilingi bilioni 1.1, sawa na Nakuru, Kiambu na Kakamega.