Mama na wanawe 2 wateketea Mombasa


Mwanamke mmoja na wanawe wawili wamechomeka hadi kufa usiku wa kuamkia leo baada ya moto kuzuka katika ploti moja mtaa wa Jitoni eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa.

Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi eneo hilo la Jomvu James Mutua anasema walipokea taarifa kutoka kwa wakaazi wa mtaa huo mida ya saa nane za usiku na wakaandamana na maafisa wa kupambana na majanga kaunti ya Mombasa na kupata moto huo tayari umesambaa katika ploti hiyo yenye vyumba 10.

Wakaazi wakisaidiana na maafisa hao walifanikiwa kuuzima moto huo lakini tayari ulikuwa umewaangamiza watatu hao kiasi cha kutojulikana.

Wakati wa mkasa huo baba ya watoto hao hakuwa nyumbani, huku mali ya thamani isiyojulikana ikiteketea katika nyumba zingine tatu.

Tayari polisi wameazisha uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha moto huo.

Miili ya watatu hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali kuu ya ukanda wa pwani.