Mama na mwanawe wafariki baada ya kupigwa na nyaya za nguvu za umeme.


Mama na mwanawe wafariki papo hapo baada ya kupigwa na nguvu za umeme katika kijiji cha Boa Matopeni eneo la Kombani huko Matuga kaunti ya Kwale mapema leo.

Kulingana na majirani walioshuhudia tukio hilo wakiongozwa na Mwanahamisi Tosha ni kwamba mwendazake amekutana na mauti yake mwendo wa kumi na mbili asubui alipokuwa akienda dukani na mwanawe wakati alipojaribu kuinua nyaya ya stima iliyoanguka barabarani wiki mbili zilizopita.

Mwanahamisi akiulaumu pakubwa usimamizi wa kampuni ya kenya power tawi la kwale kwa kuzembea katika majukumu yao kwani walipiga ripoti za kuanguka kwa nyaya hio wiki mbili zilizopita na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

Hadi kufikia sasa wawili hao bado wamekwama katika nyaya hizo kwani maafisa wa kenya power hawajafika katika eneo la tukio .