Mama afariki baada ya kuruka kutoka Abulensi


Mwanamke mjamzito na mwanawe wa umri wa miaka 2 wameaga dunia kwa njia ya kuogovya kaunti ya kajiado.

Naiso Leslie aliye na umri wa miaka 26 anaarifiwa kuruka kutoka kwa gari la kubebea wagonjwa baada ya mwanawe aliyekuwa mgonjwa kuaga dunia alipokuwa akipelekwa katika hospitali ya rufaa ya kajiado kutibiwa.

Ripoti ya polisi kuhusu kisa hicho inasema kuwa mwanamke huyo alifungua upesi mlango wa Ambulensi hiyo na kuruka nje alipobaini kuwa hali ya mtoto imekuwa mbaya.

Wote walikimbizwa hospitalini lakini mtoto akaaga dunia walipowasili hospitalini.

Mamake aliaga dunia baadaye akitibiwa kutokana na majeraha aliyopata.

Mili yao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo Ambulensi hiyo ikipelekwa katika kituo cha polisi cha Kajiado kufanyiwa ukaguzi.