‘Mala’ yasababisha balaa


Watu ishirini na Saba kutoka Kijiji cha Chelebei kata ya Changeywo eneo bunge la Mlima elgon kaunti ya Bungoma wanaodaiwa  kunywa maziwa yaliyoganda maarufu kama maziwa mala baada ya kununua kwa mama mmoja eneo hilo wamelazwa hospitalini wakiwa na maumzivu tumboni.

Akithibitisha kisa hicho, chifu wa Kata ya Changeywo Eliud Kiptalamu  amesema waathiriwa hao walianza kuumwa na tumbo na kuendesha usiku wa kuamkia leo baada ya kutumia maziwa hayo.

Chifu huyo amewataka wakaazi waliotumia maziwa hayo kujitokeza ili waweze kutibiwa.

Yanajiri hayo huku afisa Msimamizi Katika hospitali ya kaunti ndogo ya Kopsiro Kipsang Masaai akisema kuwa baadhi ya waathiriwa  waliofikishwa Katika hospitali hiyo wako salama kiafya.