Makanisa kujumuishwa kukabili Corona


Waakilishi wawili wa makanisa nchini watajumuishwa katika kamati ya kitaifa ya kupambana na janga la virusi vya Corona nchini.

Haya ni kwa mujibu wa waziri wa usalama wa ndani Dk Fred Matiang’i anayesema kuwa hatua hiyo itatoa nafasi ya makanisa nchini kutoa kauli yao kwa kuhusishwa kikamilifu katika juhudi za kuzima janga hilo.

Ameyasema haya alipoongoza mawaziri wenzake Mutahi Kagwe wa afya na George Magoha wa elimu.

Viongozi wa makanisa wakiongozwa na Dvid Oginde kutoka kanisa la CITAM ambao wameahidi kutoa kauli zao hivi karibuni.