Mahakama yadinda kuzuia utekelezaji wa kanuni mpya za kiusalama


Mahakama kuu imekataa kuzuia kwa muda utekelezaji wa kanuni za kiusalama zinazolenga mikutano ya umma iliyotolewa na baraza la kitaifa la ushauri wa kiusalama baada ya kuidhinishwa na baraza la mawaziri.

Badala yake, jaji Anthony Murima ameagiza wanaolenga katika kesi hiyo kuwasilisha majibu yaliyonakiliwa kabla ya mwisho wa siku.

Kesi hiyo itaskizwa jumatano juma lijalo.

Kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa na chama cha mawakili nchini LSK kinachopinga utekelezaji wa kanuni hizo za kiusalama.