mahakama ya Kwale yafungwa kutokana na Corona


Mahakama ya Kwale imefungwa kwa muda wa siku 10 baada ya watu watano kupatikana na virusi vya corona katika mahakama hiyo.

Shughuli za mahakama hiyo zimesitishwa kuanzia hapo jana huku zikitarajiwa kurejelewa tarehe 23 mwezi huu.

Waziri wa afya wa kaunti ya Kwale Francis Gwama amesema kuwa tayari wamenyunyiza dawa katika mahakama hiyo.