Magoha aonya walimu watakaowatimua wanafunzi wasio na karo


Waziri wa usalama wa kitaifa Dk Fred matiang’I anasema kuwa mikakati mahsusi imewekwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanarejea shuleni tarehe 4 mwezi Januari mwaka ujao.

Akizungumza katika shule ya upili ya wasichana ya Ogande kaunti ya Hoamabay, Matiangi amesema kuwa machifu wote wameagizwa kuhakikisha wanaweka rekodi ya wanafunzi wote wanaoenda shuleni wakiwemo wajawazito.

Naye waziri wa elimu prof George Magoha ameonya kuwa walimu wote watakaowarejesha nyumbani wanafunzi wasio na karo wataadhibiwa vikali.