Magari mabovu yanaswa Kisii


Magari 20 yamenaswa  kwa kosa la kutotimiza masharti ya kuhudumu barabarani katika msako uliofanywa katika barabara inayotoka Kisii kuelekea  Keroka.

Akizungumza na wanahabari baada ya shughuli hiyo, kiongozi wa kundi lililofanya  msako huo Dk Duncan Ochieng amesema kwamba magari mengi yaliyonaswa hayana  bima huku madereva wakikosa leseni.

Naye meneja wa mamlaka ya kusimamia uchukuzi na  usalama barabarani NTSA eneo hilo Aden Adou amesema kwamba wataendeleza msako huo hasa wakati huu wa sherehe za krisimasi na mwaka mpya ili kulinda wasafiri.

Wawili hao wameomba wasafiri kuwa  mstari wa mbele kuhakikisha kwamba sheria zote za usalama barabarani zinazingatiwa ili kupunguza visa vya ajali barabarani msimu huu wa sherehe.