MAENEO YA GANZE NA MALINDI KUFAIDIKA NA UFADHILI WA MIRADI YA MAJI NCHINI.


 

Shirika la kufadhili miradi ya maji nchini Water Sector Trust Fund ,limetangaza kutenga shilingi bilioni 6.5 kutekeleza miradi ya maji kote nchini.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Ismail Shaiye anadai kuwa ,Ganze na Malindi ni miongoni mwa maeneo ambayo yatanufaika pakubwa na ufadhili huo.

Katika hotuba yake baada ya kuzindua mradi wa maji eneo la Bamba ,mkurugenzi huyo amemtaka mwanakandarasi ambaye alipewa kazi hiyo ,kuukamilisha mradi huo kwa wakati ufaao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya usambazaji maji ya KIMAWASCO Hezekia Mwarua amesema, vituo vitano vya maji vitajengwa pamoja na matangi ya maji ya lita elfu tano, sehemu hiyo.

Aidha Mwarua amesema kuwa wafugaji pia ,watanufaika baada ya kujengewa sehemu kwa mifugo yao kunywa maji ,wakati wa ukame.