Madarasa kuwa na wanafunzi 20 pekee- Magoha


Waziri wa elimu Prof George Magoha anasema kuwa kila darasa litahitajika kuwa na wanafunzi wasiozidi 20 shule zitakapofunguliwa.

Akizungumza alipozuru kampuni ya kushona nguo ya KICOTEC kaunti ya Kitui, amesema kuwa serikali pia inapanga kumpa kila mwanafunzi maski mbili.

Ni mikakati anayosema serikali kupitia wizara ya elimu inafuatilia kwa karibu kuhakikisha inazingatiwa ili kuwakinga wanafunzi dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.