Madaktari waanza rasmi mgomo wa kitaifa


Chama cha madaktari nchini KMPDU kimanzisha rasmi mgomo wa kitaifa katika kaunti ya Kisii.

Katika mkao na wanahabari, kaimu katibu mkuu wa chama hicho Dk Chibanzi Mwachonda amesema kuwa wamekuwa katika mazungumzo na serikali kwa muda wa siku 36 lakini hakuna lililoafikiwa.

Chama hicho kinashinikiza masuala 11 wanayotaka yaangaziwe kuu ikiwa bima ya afya,marupurupu zaidi sawa na kuajiriwa wka madaktari zaidi.

Wameapa kuendelea na mgomo wao hadi pale matakwa yao yatakapoangaziwa licha ya tishio la kupigwa kalamu kutoka kwa waziri Mutahi Kagwe.