MACHIFU WAANGAZIE ZAIDI WANAOKIUKA KAFYU


Changamoto imetolewa kwa machifu na manaibu wao kusaidia maafisa wa polisi katika kutekeleza agizo la kafyu.
Kulingana na Richard Babu wa shirika la Uraia Trust anasema maafisa wa polisi pekee hawawezi kutekeleza agizo la kafyu hivyo machifu sharti wasaidie maafisa hao.
Babu wakati huo amelaumu viongozi wa kisiasa kwa kile anasema wanaendelea kupuuza maagizo ya wizara ya afya ya kukabili virusi vya Corona bila hatua kuchukuliwa.