MACHIFU NA MANAIBU WATAKIWA KUWAJIBIKA KUKABILI VISA VYA DHULMA-LAMU.


Machifu na manaibu wao katika kijiji cha Muamarani kaunti ya Lamu wametakiwa kuwajibika na kuona kwamba iwapo watoto wamedhulumiwa kimapenzi, basi mshukiwa wa tendo hilo anakabiliwa kisheria.

Kulingana na mwanaharakati wa kijamii Daniel Kigo, kumekuwa na changamoto kubwa eneo hilo akisema pindi watoto wanapodhulumiwa kingono, familia za pande zote mbili hukaa kwa pamoja na kumaliza kesi hizo kinyumbani.

Kigo ameeleza kuwa visa vya ubakaji dhidi ya watoto wenye umri mdogo ,ni visa vinavyoendelea kushuhudiwa hasa kipindi hiki ambapo watoto wako majumbani kufuatia janga la korona.