MABWENYENYE WAONYWA DHIDI YA UNYAKUZI WA ARDHI KILIFI.


 

Wamiliki wa ardhi katika fuo za bahari ya hindi kule Sabaki kaunti ya Kilifi sasa ,wamewaonya mabwenyenye eneo hilo dhidi ya unyakuzi wa ardhi .

Hii ni baada ya wakaazi hao kubaini kuwa baadhi ya mabwenye eneo hilo, wanafanya upimaji wa ardhi kisiri .

Kulingana na mwenyekiti wa maswala ya ardhi kule Magarini, Stembo Kaviha, kipande kimoja cha ardhi yenye ukubwa wa ekari 500 Kimeanza kushuhudia utata.

Stembo amewahimiza wahusika wote kuwashirikisha maafisa wa ardhi eneo hilo endapo ni wamiliki halisi wa ardhi hiyo ,ili kuepukana na mizozo ya ardhi.

Ni Kauli ambayo imeungwa mkono na mwanachama wa kamati hiyo Evans Katana, aliyefichua kuwa wakaazi wa sehemu hiyo sasa wanahofia kunyakuliwa kwa ardhi yao.