Mabadiliko ya uongozi kanisa la AIC


Askofu Abraham Mulwa ametawazwa askofu mkuu wa kanisa la AIC Kenya baada ya askofu Silas Yego ambaye amehudumu kwa zaidi ya miaka 40 kustaafu.

Akiongea baada ya kula kiapo, Askofu Mulwa ameahidi kuongoza Kanisa la AIC nchini kwa kuzingatia sheria na kanuni za Kanisa hilo na kushirikiana na maaskofu wengine

Askofu Paul Kirui kadhalika ametawazwa kuwa naibu askofu mkuu wa Kanisa la AIC

Askofu anayeondoka Silas Yego ameeleza kuwa mwenye furaha anapondoka madarakani sababu Kanisa la AIC limekuwa chini ya uongozi wake.

Hafla hiyo iliyofanyika katika kanisa la AIC Milimani hapa jijini Nairobi imehudhuria pia na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, naibu rais William Ruto pamoja na viongozi wengine nchini.

Rais kenyatta ametumia fursa hiyo kushukuru makanisa ya humu nchini kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kufanikisha sekta ya elimu na afya.

Amesema kuwa serikali itaendelea kuunga mkono kanisa katika juhudi za kutimiza malengo yake.

Naye naibu wake Willma Ruto amepongeza kanisa kwa mchango wake katika kuimarisha maisha ya wakenya akiahidi ushirikiano zaidi hasa kati ya serikali na viongozi wake