Maafisa walioshambulia Meru wako salama kiafya


Msimamizi wa hospitali ya rufaa ya Isiolo Dkt Hussain Mohamud anasema kuwa maafisa wa usalama waliofika katika hospitali hiyo hapo jana jioni baada ya kushambuliwa na wezi mifugo eneo la Bulû Igembe Kaskazini kaunti ya Meru wako imara kiafya, isipokuwa mmoja ambaye amepelekwa hapa Nairobi kwa matibabu maalumu.

Mohamud anasema kuwa kwa 7 waliofika katika hospitali hiyo, wawili walikuwa na majeraha madogo na walitibiwa na kuondoka huku watano wakisalia mle.

Maafisa wengine 4 wanaendelea kutibiwa katika hospitali ya kimisheni ya Maua kaunti hiyo ya Meru.