MAAFISA WA UTAWALA WA MKOA WAWE MACHO KUHUSU UKEKETAJI


Wito umetolewa kwa maafisa wa utawala wa mkoa kuwa makini msimu huu wanafunzi wako nyumbani dhidi ya swala la ukeketaji.
 
Kulingana na mkereketwa wa haki za watoto eneo la Taveta Dorcas Gibran anasema ni hatari kwa watoto wa kike kupelekwa nchini Tanzania kwa ajili ya kukeketwa na hasa wakati wa janga la Corona.
 
Gibran anasema kwa sasa wameanzisha shughli ya kuhamasisha umma kuhusu athari za ukeketaji miongoni mwa jamii za mpakani.
 
Wakati huo ametoa wito kwa bunge la kaunti kuhakikisha fedha ambazo zinatengwa kwa ajili ya kupiga vita ukeketaji zinafikia walioko nyanjani.