MAAFISA WA USALAMA KUHUSU POMBE ZA KIENYEJI- TAITA TAVETA.


Maafisa wa polisi kaunti ya Taita Taveta wamesema kwamba ,hawatachoka katika vita vya kumaliza pombe za kienyeji hasa maeneo ya mashinani.

Wanasema katika Siku za hivi karibuni ,unywaji wa pombe za kienyeji umeongezeka ,huku wakitoa wito kwa ushirikiano na wananchi.

Haya yanajiri huku maafisa wa nyumba kumi wakisema kwamba, watashirikiana nao katika kumaliza visa hivyo.