MAAFISA WA POLISI WAANZISHA UCHUNGUZI BAADA YA MWANAMUME KUUWAWA KWA KUKATWA KATWA MAPANGA-KWALE.


Maafisa wa polisi wa kaunti ya Kwale wameanzisha uchunguzi baada ya mwanaume mmoja kuuwawa na watu wasiojulikana katika eneo la Mwatate huko Kinango.

Kulingana na Kamanda wa polisi wa kaunti hiyo Joseph Nthenge ,mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 47 alifariki baada ya kukatwakatwa ,usiku wa kuamkia leo.

Akithibitisha tukio hilo, Nthenge amedokeza kwamba marehemu alifariki njiani wakati alipokuwa akipelekwa hospitalini.

Vile vile Nthenge amedai kuwa huenda marehemu aliuwawa kufuatia mzozo wa ardhi katika eneo hilo, huku akiwaonya wananchi dhidi ya kuchukua sheria mikononi ,ambapo tayari uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha mauaji hayo.