MAAFISA WA POLISI KWALE WANASA MISOKOTO 191 YA BANGI .


Maafisa wa polisi eneo la Matuga kaunti ya kwale wamefakiwa kunasa jumla ya misokoto 191 ya bangi ,yenye thamani ya shilingi takriban elfu 65, katika eneo la mteza barabara ya Lutsangani-Mbuguni huko Matuga.

Kulingana na Kamanda wa polisi kaunti ya kwale Joseph Nthenge ,hawajabaini ilikotolewa bangi hiyo na sehemu iliyokuwa ikipelekwa.

Hata hivyo amedokeza kuwa mwendeshaji bodaboda hiyo amefaulu kutoweka na kuiacha pikipiki hio pamoja na mzigo wa bangi ,baada ya kuwaona maafisa wa polisi waliokuwa wameshika doria katika eneo hilo.

Msako mkali dhidi yake umeanzishwa ,huku bodaboda hiyo ikizuiliwa katika kituo cha polisi cha kwale.