MAAFISA WA POLISI KUONGEZWA KUSINDIKIZA MAGARI, KATIKA JUHUDI ZA KUIMARISHA USALAMA LAMU.


Idara ya usalama kaunti ya Lamu imewahimiza wadau wa usafiri wa umma katika barabara ya Lamu- Garsen kuzingatia muda wanapotoa huduma  za usafiri ili kurahisisha usafiri.

Kamanda wa polisi kaunti ya Lamu Moses Mureithi amekariri idara hiyo imeweka mikakati ya kuongeza maafisa wa polisi watakao kuwa wakisindikiza magari ya umma kwa awamu ya saa sita na saa tisa ili kudhibiti usalama.

Mureithi amewataka madereva hasa wa Mombasa Kilifi na Malindi kuhakikisha wanafika eneo la Gamba kwa wakati ili waweze kupata msafara unaojumuisha maafisa wa usalama ili kurahisisha usafiri.

Hii ni baada ya kushuhudiwa msongamano wa magari katika vizuizi vya polisi mara kwa mara katika barabara hiyo wakisubiuri magari ya maafisa wa usalama ili kuwasindikiza.