MAAFISA WA KUPIMA MAJI WALETWA LAMU,KUBAINI VIWANGO VYA MAJI KUANZIA MTO TANA.


Serikali ya kaunti ya Lamu tayari imeleta maafisa wa kupima hali ya maji chini na nje ya ardhi kuanzia Mto Tana ,ulio katika kaunti ya Tana River ,lengo kuu ikiwa ni kuongeza viwango vya maji katika kaunti ya Lamu

Mwakilishi wa wadi ya Hongwe huko Lamu James Komu amesema, hatua hiyo inalenga pia kupunguza gharama za maji kwa wakaazi wa Lamu ,sawia na kutatua changamoto za uhaba wa maji unaokumba maeneo mengi eneo hilo.

Maeneo mengi ya Lamu hususan Visiwani ,wakaazi hutegemea maji ya mvua pekee ,na isiponyesha wakaazi huwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi ya kunywa , kwani visima vinavyochimbwa huwa ni vya maji ya chumvi.