Maafisa wa kliniki kurejelea mgomo


Chama cha maafisa wa kliniki kimetangaza kurejelea mgomo wao kuanzia saa sita usiku wa leo baada makataa ya saa 48  waliokuwa wamelipa baraza la magavana kutamatika.

Viongozi  wa chama hicho wakiongozwa na  Katibu George Gibore na mwenyekiti Peterson Wachira wamesema kuwa  baraza la magavana limekosa kutii mkataba wa kurejea kazini ambao ulitiwa saini tarehe moja mwezi huu.

Gibore anasema magavana hawana nia ya kuboresha sekta ya afya nchini kwani baadhi wameanza kuwafuta kazi na kuwatishia wahudumu wa afya ambao hawajarudi kazini.

Wanasema  mgomo wa sasa utaendelea hadi pale baraza la magavana litakapokuwa tayari kutia saini mkataba huo ambao unaonyesha wameafikiana kuhusu masuala 17 ambayo walikuwa wameibua.