MAADHIMISHO YA SIKU YA UTALII .


Ikiwa hii leo ni siku ya maadhimisho ya utalii,Kwa mara ya kwanza wafanyibiashara katika sekta hiyo hapa Mombasa, wameonyesha kuridhishwa na idadi ya wateja waliojitokeza kuhudhuria maadhimisho hayo, katika bustani ya Mama Ngina .

Kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya wananchi, wafanyibiashara wa Vinyago, Nguo, wachoraji Hinnah na wauzaji wa vyakula vya kitamaduni ,wamesema imekuwa afueni kwao kwa mara ya kwanza kibiashara tangu kuibuka kwa janga la Corona.

Kwenye ujumbe wao washikadau katika sekta hio wametoa wito kwa rais Uhuru Kenyatta, kuondoa marufuku yaliyowekwa kudhibiti janga la Corona, wakitaka waruhusiwe kuendelea biashara zao bila vikwazo.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla , ni pamoja na Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho, Wabunge Mishi Mboko wa Likoni, Badi Twali wa Jomvu ,Seneta wa Mombasa Mohamed Faki na Mwakilishi wa akinamama Bi Asha Hussein miongoni mwa wengine.

Hali ya usalama iliimarishwa katika uwanja huo uliojaa pomoni huku juhudi za kupima joto kwa Kila aliyefika uwanjani humo zikiambulia patupu kufuatia idadi kubwa ya watu.