“Lockdown” imesaidia sana kuzuia Covid-19


Hatua ya serikali kuzuia watu kuingia au kutoka kaunti ya Nairobi na kaunti zingine nchini imesaidia sana serikali kuzuia visa na maafa zaidi kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Katika katika wizara ya afya Dk Susan Mochache anasema kuwa serikali imekuwa ikitilia maanani ushauri wa wataalmwa kisayamsi kuhusu mkondo wa ugonjwa huo, hii ikiipa serikali mshawasha zaidi wa kuendelea kutekeleza masharti hayo ili kuwalinda wananchi.

Mochache akizungumza na Radio Citizen ndani ya mjadala wa Jambo Kenya amesisitiza kuwa serikali itakuwa makini zaidi kabla ya kulegeza masharti iliyotoa hasa kwa kuhakikisha kaunti zina uwezo zaidi wa kukabili virusi vya Corona.

Aidha amedokeza kuwa ugonjwa huo unaathiri watu kwa njia tofauti kwa kutegemea umri au hali ya afya ya mtu binafsi.