LALAMA ZA WAKONGWE KUKOSA FEDHA WALIZOTENGEWA NA SERIKALI KUU, TAITA TAVETA.


 

Imebainika kwamba baadhi ya wazee wakongwe kaunti ya Taita Taveta wangali hawajanufaika na fedha zilizotengewa wazee hao na serikali kuu.

Wazee hasa walioko vijijini maeneo ya Mwatate wanasema licha ya majina kuchukuliwa na maafisa wa utawala wa mkoa, bado hawajanufaika na pesa hizo..

Wazee hao wanasema hawajafahamu sababu ya wao kutotambuliwa na serikali, licha ya kwamba hali yao ya uzeeni haiwaruhusu kutafuta fedha za kujikimu kimaisha.