KWS INAFANYA KILA JITIHADA KUKABILI MIZOZO YA MBUGA YA TSAVO- TAITA TAVETA.


Shirika la hifadhi ya wanyamapori nchini KWS kaunti ya Taita Taveta , linaendelea kuwashawishi wakaazi wa kaunti hiyo kuunga mkono juhudi za uhifadhi wa wanyamapori.

Hii ni kufuatia madhara na hasara ,ambayo imekuwa inaendelea kusababishwa na wanyama pori eneo hilo.

Naibu mkurugenzi wa hifadhi ya mbuga ya wanyamapori ya Tsavo, Kenney Ochieng, anasema japo wanajizatiti kuhamasisha umma ,wananchi bado hawajaweza kuzingatia uhifadhi.

Kwa sasa viongozi wa Taita Taveta wakiongozwa na gavana Granton Samboja ,wanaendelea kukashifu shirika hilo na kusema ni kero kwa jamii.