Kwale yajitayarisha na COVID-19


Idara ya afya katika kaunti ya Kwale imesema kuwa imetenga vituo vitano katika hospitali mbali mbali za kaunti hii kama vyumba maalum vya kuwatenga wagonjwa walio na dalili za virusi vya corona.

Afisa mkuu wa afya katika kaunti ya Kwale Dkt. Juma Salim Mbete amesema kuwa vituo hivyo vitatumika kutenga wagonjwa.
Pia wahudumu wa afya pamoja na wafanyikazi wengine katika hospitali hizo wanapokea mafunzo ya kukabiliana kusambaa kwa virusi vya corona
Amewasisitiza wananchi dhidi ya kutoka taarifa potovu na za kuzua wasiwasi miongoni mwa mwananchi.