Kizazaa cha Nyuki Kwale.


Kizaazaa kimeshuhudiwa katika zoezi la usajili wa makurutu wa kikosi cha jeshi kufuatia uvamizi wa nyuki katika eneo la Vigurungani huko Kinango kaunti ya Kwale.

 

Kulingana na aliyeshuhudia tukio hilo, nyuki hao wamechipuka ghafla na kuwashambulia raia pamoja na maafisa wa jeshi waliokuwa wakisimamia zoezi hilo.

 

Ni hali ambayo imechangia shughuli hiyo kusitishwa baada ya maafisa wa jeshi pamoja na raia kutoroka kwa hofu ya kuvamiwa na nyuki hao.

Tukio hilo lililotokea mwendo wa saa nne asubuhi limehusishwa pakubwa na visa vya ushirikina katika eneo hilo.

Hata hivyo, kamanda wa polisi wa Kinango Fredrick Ombaka amesema kuwa zoezi hilo litaendelea baada ya hali hiyo kudhibitiwa.