Kiwango cha maambukizi ya corona chafikia asilimia 2.7


Kiwango cha maambukizi ya virusi vya corona nchini kimeshuka hadi asilimia 2.7 baada ya watu 83 kudhibitishwa kuwa na virusi kati ya sampuli 3,093 zilizopimwa.

Kwa mujibu wa waziri wa afya Mutahi Kagwe jumla ya watu walio na virusi hivyo nchini imeongezeka hadi 35, 103.

Kaunti ya Nairobi imenakili visa 27, Busia visa 15, Kisumu 12, Nakuru na Machakos visa 7 kila kaunti, Kiambu 5, Laikipia na Kisii 3, huku kaunti za Kirinyaga, Mombasa, Nyandarua, na Uasin Gishu kisa kimoja kila kaunti.

Wakati huo huo watu 72 wamepona Covid-19 , 39 wakiwa ni wale waliokuwa wakiuguzwa nyumbani.

Hata hivyo watu watatu wameaga dunia, jumla ya walioaga kufikia sasa ikiongezeka hadi  597.