Kinoti anolewa na rais Kenyatta


Rais Uhuru Kenyatta amemkosoa mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa jinai nchini DCI, George Kinoti, kuhusu hatua yake ya kufufua uchunguzi kuhusu ghasia zilizoshuhudiwa nchini wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Rais Kenyatta ameweka wazi hataruhusu uchunguzi huo kufanyika, akisema hatua hio itakuwa sawa na kuchokora vidonda vya zamani ambavyo vinaelekea kupona.

Rais Kenyatta, ambaye amezungumza wakati akizindua zoezi la kukusanya saini za BBI katika ukumbi wa mikutano KICC, amesema alisikia kuhusu mipango ya DCI kupitia vyombo vya habari.

Rais amesema maswala yalioathiri taifa hili hapo nyuma, yalipita, na sasa wakenya wagange yajayo kupitia katiba na mbinu za kisheria.

Tangazo la DCI mkuu Kinoti kwamba atafufua uchunguzi kuhusu ghasia za uchaguzi lilizua hisia huku naibu rais William Ruto na wanasiasa wanaomuunga mkono wakipinga vikali