Kindiki kubaini hatma yake alasiri


Seneta wa Tharaka Nithi Prof Kindiki Kithure anatarajiwa kubaini hatma yake katika wadhifa wa naibu spika wa bunge la senate alasiri ya leo.

Hii ni kufuatia mkao maalum ulioitishwa na spika wa bunge hilo ken Lusaka kujadili na kuamua hatma ya Kindiki.

Chama cha Jubilee kupitia kiranja wa wengi Irungu Kang’ata kimeagiza masneta wake 38 wakwiemo wenzao kutoka chama cha KANU kuhudhuria mkao huo wa leo.

Seneta huyo wa Murang’a anasema kuwa watakaokiuka agizo hilo la kumwondoa Kindiki wataadhibiwa kisheria.

Hata hivyo, kwa sasa maseneta wanaarifiwa kuwa na mkutano katika ikulu ya Nairobi wakipanga mikakati ya kufanikisha mpango huo.

Seneta Kindiki ambaye awali alihudumu kama kiongozi wa wengi katika bunge hilo anashtumiwa kwa kukosa kuhudhuria mkutano wa masesenat wa Jubilee ulioitishwa na rais Uhuru Kenyatta katika ikulu ya Nairobi, mkutano uliotumiwa kumwondoa kiongozi wa wengi Kipchumba Murkomen na kiranja wa wengi Susan Kihika.

Jubilee inahitaji maseneta 45 kati ya 67 ili kuunga mkono juhudi za kumtema Kindiki huku upande wa Kindiki ukihitaji maseneta 23 kumnusuru.

Maseneta na wabunge kutoka mrengo wa naibu rais William Ruto wamemkashifu rais Kenyatta kwa masaibu yanayomwandama Kindiki.

Kindiki amenukuliwa akikosoa woto wa kusitisha kampeni za mapema kuhusiana na uchaguzi mkuu mwaka wa 2022.