KILIO CHA MASKWOTA MWATATE-TAITA TAVETA.


Maskwota wanaoishi katika kaunti ya Taita Taveta wameitaka serikali ya kaunti hiyo kwa ushirikiano na tume ya ardhi nchini kuchukua umiliki wa mashamba yote ambayo muda wake wa umiliki ulikamilika.

Kulingana na katibu wa maskwota hao katika eneo la Mwatate Mnjala Mwaluma,amesema muda wa umiliki wa ardhi katika eneo hilo ulikamilika ,hivyo serikali haina budi kuchukua mashamba hayo.

Aidha mnjala ametaka tume ya ardhi nchini kufanya utathmini wa kina ,kuhusiana na ardhi zinazo milikiwa na watu binafsi katika eneo hilo, ili wananchi waweze kupata ardhi maalum.