KIJANA ASHAMBULIWA KWA PANGA GANZE ,KILIFI.


Hali ya sintofahamu imetenda katika Kijiji mimoja kule Ganze kaunti ya Kilifi baada ya Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 21 kushambuliwa kwa panga.

Inaarifiwa kuwa kijana huyo alikumbana na masaibu hayo kutoka kwa mamake wa kambo kwa ushirikiano na mwanawe.

Taarifa zimefichua kuwa mwanamke huyo alitekeleza tukio hilo baada ya mijana huyo kudinda kuchunga mbuzi.

Andrew Kalama kutoka Kijiji cha Tototo anadai mamake wa kambo kwa Jina Kadzo Gharama amekuwa akiwatesa yeye na nduguye wa miaka 18 tangu kuondoka kwa mama yao mwaka wa 2003.

Kalama ameeleza kuwa wanakijiji ndio walioingilia kati vita hivyo na kumkimbiza katika hospitali ya Bamba ambako anaendelea kupata matibabu.

Kulingana na Gharama Katana babake kijana huyo ambaye anadai hakuwepo siku ya mkasa huo ni kuwa, tayari walishapiga ripoti katika kituo cha polisi cha Bamba na wanasubiri kijana huyo apone ili waweze kuendelea na kesi.

Gharama pamoja na wanakijiji wameishinikiza serikali kumchukulia hatua za kisheria mwanamke huyo na mwanawe ili kijana aliyedhulumiwa apate haki yake.

Tayari Mwanamke huyo pamoja na wanawe watatu wametoroka katika Kijiji hicho hadi Bamba ambako mumewe anafanya biashara.