Kibaki na Raila wamwomboleza Mkapa


Rais Uhuru Kenyatta amemwomboleza rais wa tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa.

Katika ujumbe wake, mkapa amemtaja marehemu kama kiongozi aliyejitahidi kuhimiza amani na ustawi wa eneo hili la Afrika mashariki.

Ujumbe sawia umetolewa na rais wa tatu wa Kenya Mwai Kibaki ambaye ametaja juhudi zake katika kuleta amani katika mataifa kadha barani Afrika kama mchango mkubwa utakaoendelea kukumbukwa.

Atakumbukwa na wengi wa wakenya kutokana na mchango wake katika kuwapatisha Kibaki na kinara wa ODM Raila Odinga baada ya ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka wa 2007.

Aliandamana na aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa marehemu Dk Koffi Annan na aliyekuwa mkewe rais wa Afrika kusini Graca Machel

Ni hatua ambayo imeangaziwa pakubwa na Raila katika risala zake za rambirambi.

Rais John Pombe Magufuli alitangaza usiku wa kuamkia leo kupitia runinga ya taifa ya Tanzania taarifa za kufariki dunia kwa Mkapa katika hospitali moja jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.