Kesi zajaa pomoni Mahakamani- Maraga


Mahakama inayoshughulikia kesi kuhusi mazingira na ardhi hapa Nairobi ina kesi za kushughulikia hadi machi mwaka wa 2021 kutokana na mrudiko wa kesi katika mahakama. Mahakama hiyo pekee ina kesi 17833 ambazo hazijashughulikiwa .

Jaji mkuu David Maraga amesema kuwa mahakama inakabiliwa na mzigo mzito wa kesi ambazo bado hazijashughulikiwa kutokana na changamoto za ukosefu wa fedha .

Kulingana na ripoti ya mwaka 2018/2019 mahakama ya chini zile za mahakakimu ndizo zilizokuwa na kesi nyingi ambazo hazijaamuliwa . Kufikia mwezi juni mwaka jana ni kesi 245,256 bado zilikuwa katika mahakama hiyo ikifuatwa na makahama kuu ambapo kesi 63,433 bado hazikuwa zimeamuliwa .

Mahakama ya upeo na ile ya kadhi hazikuwa na mrundiko mkubwa wa kesi zikiwa na kesi 93 ambazo hazikuwa zimetatuliwa na mahakama hiyo ya juu ikiwemo kesi 7 ambazo zinahitaji majaji wa mahakama hiyo kutoa mwelekeo na mwongozo wa kisheria.

Kumekuwa kukishuhudiwa kesi za mauaji na kulingamna na ripoti hiyo ni asilimia 13 ya kesi za mauaji ambazo zimefikishwa mahakamani