KAUNTI YA TAITA TAVETA KUKABILIWA NA UHABA WA MADAKTARI.


Huku serikali ikijitahidi kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma za afya kote nchini,kaunti ya Taita  Taveta ingali inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madaktari.

Idadi chache iliyopo kwa sasa ya madkatari  kaunti hiyo kwa ushirikiano na wauguzi kujitolea(Community Health Volunteers)sasa wanafanya  kazi usiku na mchana kuokoa maisha ya kina mama wajawazito.

Kulingana na Timothy Wambua mmoja wa wauguzi wa kujitolea anasema kuwa hurauka asubuhi na kutembea zaidi ya kilomita 10  kuwaelimisha kina mama wajawazito na watoto kuhusu afya ya uzazi na ili kuokoa maisha.

Hatua ya Wambua na wauguzi wengine wa kujitolea kutoka kwa jamii imesaidia katika kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga wa kuzaliwa.