KAUNTI NA AJIRA KWA VIJANA,LAMU.


Mwakilishi maalum katika bunge la kaunti ya Lamu Amina Kale ameishinikiza serikali kuu na ile ya kaunti , kuangazia swala la ajira kwa vijana katika miradi inayoekezwa Lamu, ili kuwainua kiuchumi.

Katika kikao na waandishi wa habari, Kale amewasihi viongozi wa Lamu kushirikiana kwa sauti moja ,kuzungumza na kuhakikisha wanasimama kidete kupigania ajira kwa vijana hao.

Kulingana na Kale vijana wengi eneo hilo wanaendelea kuangamia kwa utumizi wa dawa za kulevya ,kutokana na ukosefu wa ajira.