KAUNTI KUWAANGALIA MAYATIMA


 

Kuna haja serikali ya kaunti ya Lamu kuwasaidia mayatima wa kaunti hiyo kwa kuwalipia karo kikamilifu ili wapate kuendeleza masomo yao kikamilifu na waweze kujitegemea wenyewe katika siku za usoni.

Hii ni kutokana na kuwa wazazi wengi wa watoto hao wamefariki kutokana na magonjwa mbalimbali ambayo yanaendelea kuangamiza zaidi wakaazi ikiwemo Saratani na ata Ukimwi huku watoto wakisalia mayatima.

Mwakilishi mteule kaunti ya Lamu Jane Wanjiku amesema vijana wengi mayataima wanakabiliwa na hali ngumu za kimaisha kwani hawana wazazi wa kuwalinda wala familia ya kuwasimamia katika maisha yao.