KAUNTI ITOE MAFUNZO KWA VIJANA TAITA TAVETA.


Changamoto imetolewa kwa serikali ya kaunti ya Taita Taveta kutoa mafunzo maalum kwa vijana kuhusu jinsi ya kujiendeleza kibiashara.

Kulingana na vijana kaunti hiyo wanasema, makali ya Covid 19 yamewaacha wengi bila ajira ,na sharti wapewe mafunzo maalum ya kujikwamua kibiashara.

Aidha wanatoa wito kwa kaunti kuunda hazina maalum ya kusaidida vijana hao.