Kaunti 11 zapitisha mswada wa BBI


Kaunti ya Laikipia imekuwa kaunti ya kwanza eneo pana la Mlima Kenya kupitisha mswada wa mabadiliko ya katiba kupitia BBI.

Waakilishi wadi wa kaunti hiyo kwa kauli moja wamepitisha mswada huo wakielezea umihimu wake kwa wananchi kupitia mapendeekzo yake.

Kaunti ya Nairobi jioni hii pia imepitisha mapendeekzo ya mswada wa mabadiliko ya katiba kwa kauli moja.

Ni uamuzi ambao umeshabikiwa pakubwa na seneta wa Nairobi Johnson Sakaja,mbunge wa Makadara George Aladwa na mbunge mteule Maina Kamanda.

Kaunti hizo sasa zinajiunga na kaunti zingine kama vile Vihiga, Kisii, Trans Nzoia, West Pokot, Busia, Homa Bay, Kisumu na Siaya ambazo tayari zimepitisha mswada huo.