Katibu mkuu wa KMPDU


Kaimu katibu mkuu wa chama cha madaktari humu nchini Dk Chibanzi Mwachonda amethibitishwa kuwa na virusi vya Corona.

Katika taarifa, mwachonda amesema aliambukizwa virusi hivyo alipokuwa akitekeleza kazi rasmi.

Hata hivyo anasema kuwa hali yake kiafya iko sawa akiwa karantini.

Mwachonda anasema kuwa ugonjwa huo wa Covid-19 uko katika jamii hivyo basi kila mmoja anafaa kuwa makini zaidi.

Amewataka wananachi kuzingatia masharti ya wizara ya afya ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi hivyo.