Kampuni za usafiri zasitisha safari za usiku .


Kufuatia agizo la rais la kutotoka nje mwendo wa moja jioni hadi kumi na moja alfajiri kampuni nyingi za mabasi ya masafa marefu zimebadilisha muda safari zake.

Kampuni hizo ikiwemo Modern Coast, Dreamline na Mash zimesema kuwa sasa hazitafanya kazi nyakati za usiku.

Aidha katika taarifa yake mabasi yake yataondoka kati ya mwendo wa saa mbili asubuhi hadi saa tatu na robo.

Wasafiri ambao wameathirika wamehimizwa kuwasiliana na kampuni husika ili waweze kujulia kuhusu safari zao.