Kampeni za uchaguzi mdogo Taita zangoa nanga.


Huku kampeni za uchaguzi mdogo wa wadi ya Wundanyi Kaunti ya Taveta zikianza, Peter Mwabili wa chama cha Ford Kenya amewasilisha stakabadhi zake kwa tume ya IEBC kuwania kiti kilochobaki wazi baada ya kifo cha dadake Beatrice Mwabili aliyekuwa mwakilishi wa wadi hiyo.

Akihutubia waandishi wa habari baada ya kupokea cheti rasmi cha kugombea nafasi hiyo, Mwambili ameapa kuendeleza kampeni ya amani na inayozingatia maswala muhimu na sio siasa za chuki.

Afisa mkuu wa IEBC eneo bunge la Wundanyi Margaret Mzae amesema wagombeA kumi na tano wanatarajiwa kuwasilisha vyeti vyao kufikia mwisho wa siku hii.

Naye mshirikishi wa Kitaifa wa Chama cha Ford Kenya Chris ManduMandu amesema chama hicho kimeweka mikakati ya kuhakikisha mgombea huyo na wengine katika chaguzi ndogo kote nchini wanapata nafasi wanazo wania.